Ushindi wake umeshangaza wengi. Waliokuwa wanatarajiwa zaidi kushinda tuzo hiyo ni Diamond na Wizkid. Na kwa mashabiki wengi wa Diamond, Wizkid ndiye waliyekuwa wakimhofia zaidi. Lakini tulikuja kujipa moyo kuwa huenda mwaka huu ushindi ni wetu kutokana na msimamo wa Wizkid dhidi ya tuzo hizo za Wamarekani.
Mwaka jana alieleza sababu ya kutohudhuria akidai kuwa haziwapi heshima wasanii wa Afrika na UK. Na tangu atajwe kuwania tuzo hizo, hajawahi kujali, kusema chochote na hakuhudhuria kabisa. Hivyo nafasi kubwa ilionekana kwenda kwa Chibu. Hata hivyo, BET waliamua kumpa Black Coffee – Dj ambaye jina lake ni geni kabisa kwa Watanzania wengi.
“For the past 4/5 years I have been doing tours outside my Country…..in the last two years even relocating my Family with me while on tour to make everything work…..Taking our South African Music to places I can’t even pronounce,” aliandika kwenye Instagram baada ya ushindi huo.
“I’m Greatful to my lady @enhlembali_ and my kids for allowing me to chase my dreams unconditionally…….my great team @amarudacosta @lionelmarciano and both offices in SA and NY….Universal Music team in SA…..Ultra Music team in NY and the William Morris Team in LA…..a BET Award comes to our our Land for the first time.This is a Great Honour…..We did not do this alone…Thank you for all your Votes…..Thank you for the Love. #betawards16 #bestinternationalaact2016 #gotnothingbutloveformypeople #southafica #onemanband #Godsveryown #california #itsallpossible,” aliongeza.
Diamond alimpongeza pia kwa ushindi huo. Lakini pamoja na jina lake kutokuwa kubwa katika upande mwingine wa Afrika, ukitoa Kusini, Black Coffee ni legend ambaye katika wote aliokuwa ametajwa nao, yeye ndiye kaka yao.
Black Coffee ni nani?
Jina lake halisi ni Nathi Maphumulo. Ni Dj mwenye mkono mmoja. Alipoteza mkono wake baada ya taxi kuanguka kwenye kundi la watu ambalo naye alikuwemo, mtu mmoja alikufa na Black Coffee alikuwa mmoja wa watu 36 waliojeruhiwa.
Ajali hiyo ilimfanya Maphumulo apoteze mkono mmoja ambao umejikunja kama ngumi na kuwa mfukoni mara nyingi. Mkono wake wa kushoto siku zote huwa upo mfukoni na bado akiwa na miaka 35, amefanikiwa kuwa na mafanikio ambayo wengi katika umri huo hawana.
Lakini hakukata tamaa ya kuwa DJ mkubwa ambapo alijiunga na chuo cha Durban Tech kusomea music production. Kwa sasa Black Coffee ni mmoja wa majina yanayoheshimika kwenye muziki wa dance nchini Afrika Kusini na kimataifa pia.
Black Coffee hajawahi kutaka kujulikana kama ‘DJ mwenye mkono mmoja’ kwakuwa anapenda atambulike kwa kipaji chake na sio kwa ulemavu wake. Alifungua label yake iitwayo Soulistic Music na ameshacheza muziki katika maeneo mengi yakiwemo Uingereza, Marekani, Ugiriki na kwingine duniani na huko anaheshimika mno.
0 comments:
Post a Comment