Drama kwenye tuzo za BET ziliendelea tena mwaka huu. Kama kawaida,
Wizkid alizipa mikausho mikali kwa si tu kwa kugoma kwenda kama wengine,
bali hata kuzizungumzia kabisa. Lakini imebainika pia kuwa AKA na Yemi
Alade walitoa mikausho yao. Yemi hakwenda kwenye utoaji wa tuzo katika
vipengele vya Best International Act: Afrika na UK. Lakini AKA yeye
anadaiwa kuwa alikuwepo ukumbini hapo lakini hakupanda jukwaani kama
wengine.
Diamond, Cassper Nyovest na Black Coffie walikuwepo. Kutokana na kitendo
hicho kumekuwepo na mjadala mkubwa Afrika Kusini kuwa AKA hakupenda
ushindi wa Black Coffee ambaye wamewahi kutupiana vijembe kwenye Twitter
kipindi cha nyuma. Hata Hivyo AKA amekanusha na amempongeza DJ huyo.
Monday, 27 June 2016
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment